Bei mpya za mafuta, Petroli na Dizeli zashuka

HomeKitaifa

Bei mpya za mafuta, Petroli na Dizeli zashuka

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo ya mafuta ya petroli, dizeli na taa ambapo bei imepungua kwa Sh 187 kwa lita ya petroli itakayo pakuliwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Pia Bei ya Dizeli imepungua kwa Sh 284 kwa lita na Bei ya mafuta ya taa imepungua kwa Sh 169 kwa lita ukilinganisha na bei inayotumika sasa iliyotangazwa Machi 1, 2023.

Kwa Mikoa yya Kaskazini (Tanga, Arusha na Manyara), bei za rejareza zilizotangazwa na Mamlaka leo Aprili 4, 2023 zimepungua kwa Sh 158 kwa lita ya Pettroli, na Sh 231 kwa lita ya Dizeli.

Bei ya rejareja ya Petroli kwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambayo hupokea mafuta kupitia Bandari ya Mtwara, imepungua kwa Sh 220 kwa lita na Sh 176 kwa lita ya Dizeli.

CAP PRICES FOR PETROLEUM PRODUCTS EFFECTIVE WEDNESDAY 5th APRIL 2023
error: Content is protected !!