Zijue njia 7 za kuzuia kunyonyoka nywele kwa wanaume

HomeElimu

Zijue njia 7 za kuzuia kunyonyoka nywele kwa wanaume

Tatizo la kunyonyoka nywele ni tatizo linalowakumba wanaume wengi duniani. Takwimu zinaonesha kwamba tatizo hili huathiri theluthi moja ya watu duniani kote ambapo mtu mmoja hupoteza nywele 100 kila siku.

Ziko njia nyingi zichangiazo upotevu wa nywele kwa Wanaume, njia hizo ni pamoja na matumizi ya dawa za nywele bila ushauri wa kitaalamu na mabadiliko ya homoni mwilini, msongo wa mawazo, kuchafuka kwa hali ya hewa, vinasaba, kupenda kuvaa kofia muda mrefu au kuvaa muda mrefu.

Upotevu wa nywele hutokea kwa kasi tofauti, hii ni kulingana na mtu, mwingine hupoteza nywele polepole na mwingine hupoteza nywele kwa haraka zaidi na kuacha upara katikati na pembezoni mwa kichwa. Tatizo hili ni kubwa zaidi kwa wanaume kuliko wanawake.

Mabadiliko haya huja kwa kushtusha mara nyingine, hupoteza muonekano wa mtu na wengine kufikia kutokuwa na furaha na mabadiliko wanayopitia, hadi kuzoea, inachukua muda kidogo. Sasa zipo njia za kitaalamu ambazo mtu anashauriwa kuzitumia kupunguza tatizo la kunyonyoka nywele.

  1. Kula kwa wingi vyakula vyenye protini
    Vyakula kama nyama, samaki, maharage na jamii nyingine za vyakula vya protini hupunguza sana upotevu wa nywele kichwani. Protini hufanya nywele zako ziwe imara na kutopotea kwa urahisi pindi utakapozitana na kuvaa kofia.
  2. Kanda kichwa chako kwa mafuta maalum
    Kichwa ni sehemu muhimu sana kwenye miili yetu, ni lazima kila unachotaka kufanya kwenye kichwa chako uwe makini sana, ikiwezekana omba ushauri kuepusha madhara makubwa ambayo yanaweza kutokea. Wapo wataalamu wenye vyeti wanaokanda vichwa kwa mafuta maalumu kama ya mzaituni, almondi au mafuta ya sesame. Kufanya hivi mara kwa mara kunaimarisha afya ya nywele zako na kupunguza sana upotevu wa nywele.
  3. Epuka kutana nywele zilizoloana
    Kupenda kutana nywele zenye maji ni moja ya sababu inayochangia sana upotevu wa nywele. Hupaswi kuwa na haraka utokapo kuoga au kunawa kichwa, chukua taulo lako na tumia muda kukausha kichwa chako kisha acha kipigwe na hewa kikauke vyema. Nywele zikiwa na maji huwa laini, ni rahisi kukatika kama zitakutana na kitana. Na kama utazitana zikiwa zimeloa, basi hakikisha kitana chako kina njia pana zitakazoshika nywele zako.
  4. Juisi ya vitunguu maji, vitunguu swaumu na maji ya tangawizi
    Tumia bidhaa moja wapo kati ya hizo hapo juu kukabiliana na tatizo. Usichanganye, tumia moja wapo. Pakaa kwenye kichwa chako kabla ya kulala usiku, kisha lala nayo hadi asubuhi na osha kwa maji ya kawaida. Fanya hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja hakika utapata matokeo ya haraka kwenye nywele zako.
  5. Kunywa maji mengi
    Hakikisha mwili wako haukosi maji. Maji ni kitu muhimu sana kwenye kutunza afya ya nywele zako pamoja na kuzifanya ziwe imara wakati wote. Hakikisha unakunywa angalau glasi nane za maji kwa siku.
  6. Usivute Sigara
    Uvutaji wa sigara kupelekea mwili kupunja kiwango cha damu ambacho kinapaswa kufika kwenye kichwa, na kama tunavyojua damu ndio hubeba virutubisho mwili na kuvisafirisha maeneo mbalimbali mwilini. Kwa mantiki hiyo, matumizi ya sigara na vilevi vingine ni hatari sana kwa makuzi ya nywele zako, na inashauriwa kuwa ili kutunza nywele zetu vizuri, hatuna budi kuachana na matumizi ya sigara na ulevi wa aina nyingine.
  7. Epuka msongo wa mawazo
    Tafiti zinaonesha kuwa upo uhusiano wa karibu zaidi kati ya kunyonyoka nywele na msongo wa mawazo. Njia moja wapo ya kupunguza mawazo ni kufanya mazoezi, kujichanganya na marafiki na hata kusoma vitabu. Msongo wa mawazo husimamisha uzalishaji wa madini yanayosaidia nywele kuota, baada ya muda nywele huanza kunyonyoka kirahisi sana hata kwa kuosha, kutana au kuzigusa.
error: Content is protected !!