Polepole apoteza uenyekiti kamati ya Bunge

HomeKitaifa

Polepole apoteza uenyekiti kamati ya Bunge

Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), amefanya mabadiliko madogo ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 135 (3) – (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni 2020. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

  1. Mhe. Godwin Emmanuel Kunambi anahamishwa kutoka kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenda kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
  2. Mhe. Humphrey Hesron Polepole anahamishwa kutoka Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenda Kamati ya Sheria Ndogo.
  3. Mhe. Asia Abdulkarim Halamga ameteuliwa kuwa Mjumbe ya Kamati ya Masuala ya UKIMWI.
  4. Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo na kamati ya Masuala ya UKIMWI.
  5. Mhe. Dkt. Medard Matogolo Kalemani ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo.
  6. Mhe. Eng. Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo; na
  7. Mhe. Agnes Mathew Marwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI.
error: Content is protected !!