Leo katika historia: Shirika la posta duniani lilianzishwa

HomeElimu

Leo katika historia: Shirika la posta duniani lilianzishwa

Leo, tarehe 9 Oktoba ni Siku ya Kimataifa ya Shirika la Posta duniani. Posta ndio chombo cha kale zaidi na kikubwa cha mawasiliano baina ya watu wa nchi na maeneo mbalimbali ya Dunia. Taasisi ya posta ilianzishwa tarehe 9 Oktoba 1874 na ni miongoni mwa asasi za kijamii zilizobakia hai hadi leo.

Kufuatia wiki ya maadhimisho ya siku ya Posta duniani, Shirika la Posta mkoa wa Dar es Salaam tarehe 06, Oktoba 2021, limetembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa kutoka katika hospitali za Muhimbili na Ocean Road.

Wagonjwa waliopata misaada hiyo ni pamoja na watoto wenye matatizo mbalimbali na wagonjwa wa Saratani.

Tukio hilo lililoongozwa na Meneja wa Posta mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Arubee Ngaruka, ni kati ya matukio mbalimbali yanayofanyika wiki hii, ikiwa ni shamrashamra za kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Posta duniani ambayo hufanyika tarehe 8 na 9 Oktoba ya kila mwaka, huku mwaka huu yakifanyika kwa mara ya 52.

error: Content is protected !!