Mastaa wa Bongo waliobarikiwa watoto 2021

HomeBurudani

Mastaa wa Bongo waliobarikiwa watoto 2021

Mwaka 2021 umekuwa na baraka kwa mastaa mbalimbali wa Bongo kwa kubarikiwa kupata watoto na wengine kuzidi kuongeza familia zao. Mastaa hao ni wanamitindo, waigizaji, wafanyabiashara na wanamuziki.

Hii hapa orodha ya mastaa hao waliopata watoto mwaka huu hapa,

1. Tunda na Whozu
Tunda Sebastian maarufu kama Tunda na mpenzi wake Whozu, ambaye ni msanii kutoka label ya Too Much Money walibarikiwa kupata mtoto wa kike waliyempa jina la Lola. Lola alizaliwa Juni 29.

2. Vanessa Mdee na Rotimi
Staa huyu aliyewahi kukimbiza kwenye Bongo Fleva kabla hajaamua kuacha muziki, alipata mtoto  wa kiume mwezi Septemba mwaka huu. Vanessa na mchumba wake Rotimi wamempa mtoto huyo jina  Seven.

3. Amber Lulu na Botion
Mwezi machi mwaka huu wawili hao walipata mtoto wa kike na kumpa jina la Ariana. Kwa sasa wawili hao hawapo pamoja kama wapenzi bali wazazi walezi wa mtoto huyo.

4. Elizabeth Michael na Majizzo
Msanii huyu wa filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amepata mtoto na mume wake Francis Ciza ‘Majizzo’ ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha  TV E na redio EFM July 16. Jina halisi la mtoto huyo halijawekwa hadharani, badala yake anajulikana kwa ufupisho kama ‘G’.

5. Malkia Karen
Huyu ni mtoto wa mtangazaji maarufu nchini Tanzania , Gadner G Habash, pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ametangaza rasmi Oktoba 27 kuwa amejifungua mtoto wa kiume anayeitwa Caleb. Bado Karen hajaweka wazi baba mzazi wa mtoto huyo.

6. Jacquline Wolper na Rich Mitindo
Tarehe 7 mwezi Mei wawili hao walibarikiwa kupata mtoto wa kiume anayefahamika kama Pascal na waliamua kumficha mtoto huyu mpaka siku aliyotambulishwa kama balozi wa Sweet Lorah (duka la nguo za watoto).

error: Content is protected !!