Adaiwa kujaribu kuwaua watoto wake kisha kujinyonga

HomeKitaifa

Adaiwa kujaribu kuwaua watoto wake kisha kujinyonga

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40 kutokea kaunti ya Kericho nchini Kenya alijaribu kuwaaua watoto wake wawili na kisha kujinyonga, Mwanamke huyo inadaiwa aliwalazimisha watoto wake kunywa dawa ya kuua kupe na utitiri kabla ya kujitoa uhai wake.

Kwa mujibu wa majirani walisema kuwa watoto hao walipiga kelele zilizofanya majirani waende kuwaangalia, walipofika walijaribu kuwauliza ili kujua kilichotokea lakini watoto hao walishindwa kujibu kwani walipoteza fahamu muda mfupi baadaye huku mama yao akiwa amejinyoga kwenye mti uliopo nyuma ya nyumba yao.

Watoto hao walikimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Koru, ambako inasemekana hali zao zinaendelea vizuri, Bado haijulikani ni nini kilitokea kabla ya tukio hilo la kushangaza lakini Maafisa kutoka kituo cha polisi cha Fortenan walihamisha mwili wa mwanamke huyo kwaajili ya mazishi.

error: Content is protected !!