Mitego 380 yateguliwa hifadhi ya Taifa ya Nyerere

HomeKitaifa

Mitego 380 yateguliwa hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Wizara ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kutegua nyaya za umeme 380 zilizokuwa zimetegwa katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere iliyopo mkoani Morogoro ikiwa ni aina mpya ya ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumza hivi karibuni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kufadhili mradi huo wa kunasua mitego iliyotegwa kwa ajili ya kuua wanyamapori katika hifadhi hiyoWaziri Dkt Ndumbaro amesema Majangili wamekuja na mbinu mpya mara baada ya Serikali kupambana na ujangili wa biashara ya wanyamapori wakubwa kama vile Tembo na Faru.

Ameeleza kuwa ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo kwa kutumia nyaya za umeme umeanza kuchukua sura mpya huku Serikali ikiahidi kuendelea kupambana na mbinu hiyo.Dkt. Ndumbaro amesema tangu kuundwa kwa kikosi maalumu kwa kushirikiana na Wanavijiji kwa ajili ya kutegua mitego hiyo jumla ya wanyamapori watatu walikutwa wamekufa mara baada ya kunaswa kwenye mitego hiyo.

Wanyamapori waliokutwa wamekufa kuwa ni Twiga mmoja pamoja na Swala wawili hata hivyo Dkt. Ndumbaro amesema kupitia mradi huo wa kunasua mitego Wizara hiyo imekuja na mbinu ya kuwashirikisha wanavijiji wanaopakana na hifadhi kwa ajili kupambana na majangili hao.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mhe. Regine Hess amesema Serikali yake iliamua kufadhili mradi wa kutegua mitego hiyo baada ya Serikali ya Tanzania kufanikisha kukomesha ujangili kwa asilimia 90 hususan ujangili wa biashara.

Balozi Hess ameleezea kuwa mradi huo pia umeonesha mafanikio makubwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo mitego mingi imeweza kuteguliwaAidha, Balozi huyo ameipongeza Serikali ya Tanzania kuwa Serikali ya kwanza Barani Afrika kwa kusimamia shughuli za uhifadhi kiukamilifu

error: Content is protected !!