Prince Harry akiri kumuonya Bosi wa Twitter

HomeKimataifa

Prince Harry akiri kumuonya Bosi wa Twitter

Prince Harry kutoka kwenye familia ya Malkia wa Uingereza, ametamka kuwa aliwahi kumuonya mmiliki na mkurugenzi wa mtandao wa Twitter, Jack Dorsey kupita barua pepe kuwa, mtandao wake unatumika na watu kupanga mashambulizi.

Prince Harrya alisema kuwa alimtumia Dorsey ujumbe huo kabla ya Januari 6 ambapo wafuasi wa Rais wa Marekani aliyepita Donald Trump hawajavamia Bunge la Marekani na kufanya uharibifu.

Tukio la raia nchini Marekani kuvamia Bunge na kusababisha vifo vya watu watano, lilipangwa na kuhamasishwa sana kupitia mtandao wa Facebook na Twitter ambapo uchunguzi wa kina unaendelea kwa sasa kufuatia tukio hilo.

Harry kwa sasa anafanya kazi Shirika la ‘Think Tank Aspen Institution’ na kazi yake nyingine ni kutazama upotoshaji wa taarifa mitandaoni na madhara yake kwenye jamii.Aliseme, “Mmi na Dorsey tulitumiana barua pepe, na nilimuonya kuwa Twitter inatumika vibaya, alinisikia, lakini tangu nimwambie hivyo hakunirudia tena kwa ujumbe kwa punde lile nililo tabiri limetokea”.

error: Content is protected !!