Wagonjwa wa Presha hatarini kupata matatizo mfumo wa fahamu

HomeKitaifa

Wagonjwa wa Presha hatarini kupata matatizo mfumo wa fahamu

Watafiti kutokea nchini Tanzania wamebaini wagonjwa wanaougua shinikizo la damu (blood pressure) la muda mrefu wapo hatarini kupata mabadiliko ya mfumo wa fahamu ikiwemo kupungua kwa uwezo wa ubongo kufikiri, kuweza kuongea au kuwa na kauli sawasawa pamoja na kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu na umakini.

Dkt Pedro ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) amesema waliangalia mabadiliko yanayotokea katika ubongo na kwa namna gani wagonjwa wanapata matokeo hasi kupitia ugonjwa huu.

Dkt Pedro ameeleza kuwa walitumia dodoso ambalo linatumika katika kupima uwezo wa ubongo ‘PCOG’ kwa kuwahoji wagonjwa 1,201 na kwa ujumla asilimia 43.6 ambayo ni sawa na wagonjwa 524 walikutwa na mabadiliko hasi lakini pia ilibainika elimu inachangia katika mabadiliko ya ubongo.

Hata hivyo wataalamu  wametahadharisha kuwa watu wanapaswa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kujua na kuepuka madhara yatokanayo na ugonjwa huo.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa ni asilimia 10 pekee ya wenye shinikizo la damu nchini wanajua kuhusu hali zao lakini takwimu za Taasisi ya Moyo na Jakaya Kikwete (JKCI) pekee zikionesha uwezekano wa tatizo kuwa ni kubwa zaidi  kwani takwimu hizo zinaonesha kati ya watu 10 wanaoanza matibabu ya moyo Sita hukutwa na shinikizo la damu bila wao kujua. huku kwenye kila Wanawake wanne mmoja ana shinikizo la moja na kwa wanaume kwenye kila wanaume watano mmoja ana tatizo hilo.

error: Content is protected !!