R. Kelly ahukumiwa miaka 20 jela

HomeKitaifa

R. Kelly ahukumiwa miaka 20 jela

Mwimbaji wa Marekani Robert Kelly, maarufu R. Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.

Kesi zisizoisha zimekuwa zikimwandama mwamba wa nyimbo maarufu ya ’ I believe I can Fly’, Robert Kelly, au maarufu R. Kelly.

Kelly alishtakiwa kwa kuwanyanyasa kingono watu 4, 3 wakiwa watoto, katika kesi hii na alikabiliwa na mashtaka ya ponografia ya watoto. Alipatikana na hatia katika mashtaka 6 kati ya 13, huku mahakama ikimtia hatiani kwa makosa ya ponografia ya watoto, lakini ikamwachia kwa mashtaka ya kula njama na kushawishi.

 

error: Content is protected !!