Samia apeleka kicheko Katavi

HomeKitaifa

Samia apeleka kicheko Katavi

Wananchi wa Kijiji na Kata ya Inyonga Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wameishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu ambapo imewawezesha baadhi ya vijana na wazee kujipatia ajira na kujiwezesha kiuchumi.

Kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kupitia mradi wa Maji Inyonga unaotekelezwa na Wakala wa Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umewasaidia wananchi hao kujiajiri kwa kuchota maji ya bomba kwa kiasi cha Sh 50 kwa dumu la maji lenye lita za ujazo 20 na kuyauza mtaani kwa njia ya toroli kwa Sh250.

“Mradi huu wa maji tiririka ni mzuri kwasababu hatuchoki kupampu maji kama zamani tulipokuwa tunatumia maji ya visima, tunamshukuru mama Samia kutuletea mradi huu”alisema Jumanne mkazi wa Inyonga.

Hata hivyo kupitia mradi huo ulio chini ya RUWASA Wilaya ya Mlele wapo vijana waliojenga makazi ya kuishi kupitia kazi ya kuuza maji ya bombani.

error: Content is protected !!