Pochi la Rais Samia lafunguka Idodi

HomeKitaifa

Pochi la Rais Samia lafunguka Idodi

Changamoto za huduma ya afya za wananchi wa Iringa zimefika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Rais Samia Suluhu nae akusita kuboresha kituo cha afya katika kata ya Idodi, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. 

Kituo hicho cha afya kinahudumia kata mbili ambazo zinakadiriwa kuwa na watu takribani 14,630.

Kituo cha afya Idodi kinatoa huduma zote muhimu ikiwemo huduma za upasuaji, uongezaji wa damu na huduma za uzazi ambao wananchi walilazimika kuzifata mbali kabla ya uboreshaji wa kituo hiko jambo ambalo lilihatarisha maisha ya wagonjwa kutokana na changamoto za barabara na umbali wa kufika hospitalini.

Erasto Mapunda. dereva wa gari la kubebea wagonjwa wa dharura anasema kuna muda ilimchukua siku mbili mfululizo akiwa kuendesha gari bila kupumzika, Erasto ilibidi awe anahamisha wagonjwa kutoka kata hiyo na kuwapelekwa hospitali kubwa ambako wangeweza kupatiwa matibabu.

Wakazi wa Idodi wanatoa shukrani zao kwa Rais Samia kwa kuwezesha upatikanaji huduma za afya bora karibu na makazi ya wananchi, nae Mganga Mfawidhi wa kituo hiko Dkt Frank Kitumbika amesema kwa sasa wanaweza kufanya upasuaji kwa urahisi ambazo zinawanufaisha wananchi.

Wakazi wa Idodi wamefutwa machozi na kuwekea alama na Rais Samia katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja tangu awe madarakani

 

error: Content is protected !!