Anayesadikiwa kuua wanae azimia

HomeKimataifa

Anayesadikiwa kuua wanae azimia

Baba wa watoto watatu wa Shule ya Msingi Ratanda na Shule ya Sekondari ya Khanya Lesedi waliofariki dunia baada ya kupewa ‘energy dink’ (kinywaji cha kuongeza nguvu) akutwa akiwa amezimia nyumbani kwake Heidelburg – Gauteng, Afrika Kusini.

Kati ya ndugu hao watano, wanne walianza kulia na kulalamika kuumwa na tumbo kabla ya kudondoka na kupoteza fahamu. Wawili walifia shuleni, mmoja alifia njiani akipelekwa hospitali na wa nne ana hali mbaya hospitalini huku watano akiponea kwai hakuwa amekunywa kinywaji kile.

Baba huyo aliwapatia watoto wake wote energy drink inayosemekana kuwekewa sumu ndani yake asubuhi wakijiandaa kwenda shuleni baada ya mama yao kuelekea kazini.

Polisi wakimkuta baba huyo nyumbani kwake akiwa amejizidishia dozi za dawa na kujichoma kisu baada ya kusikia taarifa za msiba wa wanae na kukimbizwa hospitali ambapo amewekwa chini ya uangalizi wa polisi.

Mwakilisi wa Bodi ya Elimu Gauteng amesema kifo cha watoto hao kinaonekana kuwa kimekusudiwa lakini pia Wizara ya Elimu itashughulikia mazishi ya watoto hao.

watoto waliofariki ni Lehlogonolo Khoabane (16), Katleho Khoabane (13) na Tebogo Ngcongwane (6).

error: Content is protected !!