Afrika Kusini kuwa na lugha za Taifa 12

HomeKimataifa

Afrika Kusini kuwa na lugha za Taifa 12

NCHI ya Afrika Kusini ni ya tatu duniani kwenye orodha ya nchi zenye lugha za Taifa nyingi zaidi kwa kuwa na lugha 11 na bado namba hiyo inaongezeka.

Baraza la Mawaziri Afrika Kusini hii leo, Mei 26, 2022 limepitisha mswada wa kurekebisha kanuni ya 18 ya katiba ili kuongeza lugha ya alama ya nchi hiyo (South African Sign Langauge (SASL) kuwa lugha ya 12 kwenye orodha ya lugha rasmi za Taifa hilo.

Mswada huo wa kuipitisha lugha hiyo unasubiria saini ya Rais Ramaphosa ili nchi hiyo kutimilisha lugha dazeni moja.

Kuongezwa kwa ugha hiyo ambayo ilianza kufundishwa kama somo mojawapo ya masomo ya lazima kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutasaidia kurahisisha mawasiliano baina ya wenye uhitaji maalum na wananchi wengi wa Afrika Kusini.

Lugha nyingine 11 za nchi hiyo ni pamoja na;

Kiingereza
Afrikaans
IsiZulu
IsiXhosa
Sepedi
SeTswana
SeSotho
XiTsonga
SiSwati
TshiVenda
Ndebele (Transvaal Ndebele)

Bolivia ndio nchi yenye lugha za Taifa nyingi zaidi (37) ikifuatiwa na Zimbabwe yenye lugha za Taifa 16.

error: Content is protected !!