Mapendekezo ya Wanangorongoro

HomeKitaifa

Mapendekezo ya Wanangorongoro

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea mapendekezo ya wananchi wa Tarafa za Loliondo, Ngorongoro na Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo.

Aidha, amesema kuwa ujenzi wa makazi mapya Msomero, Tanga ya wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiari unaendelea vizuri.

Waziri Mkuu amesema nyumba 103 zipo mbioni kukamilika, pia srikali imepanga kuongeza nyumba 307 ili kufikia nyumba 500 kwa ajili ya wakazi hao.

Amemaliza kwa kusema kuwa serikali inaendelea kuimarisha sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wote nchini wanapata tija kupitia shughuli hiyo.

error: Content is protected !!