Mbinu 4 za kutumia upandishwe cheo kazini

HomeElimu

Mbinu 4 za kutumia upandishwe cheo kazini

Unapokua mfanyakazi pamoja na kulipwa mshahara na stahiki zote lakini ni matarajio ya wengi kuona wanakua katika maeneo yao ya kazi. Hivyo ili uweze kupandishwa cheo unatakiwa kufanya yafuatayo:

Watazame watu waliowahi kupandishwa cheo
Unatakiwa kuangalia watu waliowahi kupandishwa cheo tabia zao kazini zikoje, changamoto na mafanikio yao wakiwa kazini. Hii itakusaidia kujua nini unatakiwa kufanya ukiwa kazini na tabia gani uwe nazo kazini.

Jitahidi utambulike kwenye eneo lako la kazi 
Ili kuwaaminisha wafanyakazi wenzio na muajiri wako kama unastahili kupandishwa cheo lazima waone mchango wako, nini unafanya kazini kwa kujitolea inapotokea kuna mpango unatakiwa kufanyika na kampuni, angalia fursa ziliozopo kazini zinazohitaji uwezo wako na waulize wafanyakazi wenzio kuhusu ufanyaji kazi wako.

Maagizo ya Serikali kwa mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania

Onyesha uwezo wako wa kuongoza
Ikiwa unatarajia kuwa na cheo kikubwa waoneshe kuwa unaweza kuongoza, kuwa sehemu ya mtu anaeangaliwa na wafanyakazi wenzio pia unapopata nafasi ya kusimamia kitu simamia ipasavyo.

Ongeza ujuzi wako
Ni vizuri kujitahidi kujifunza vitu vipya vinavyoendana na kazi yako kwa kusoma kozi mbalimbali, kuhudhuria semina na warsha mbalimbali pia jifunze kwa wengine kwa kufuatilia wanajua nini ambacho wewe haujui.

error: Content is protected !!