Soma hapa ufafanuzi wa TANESCO kukosekana huduma ya LUKU

HomeBiashara

Soma hapa ufafanuzi wa TANESCO kukosekana huduma ya LUKU

Hitilafu imetokea kwenye mfumo wa ununuzi wa umeme wa LUKU wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), hivyo kusababisha wateja kushindwa kupata huduma hiyo muhimu.

Taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa hitilafu hiyo imetokea leo Oktoba 4, 2021, na wamewaomba wananchi radhi kutokana na tatizo hilo lililosababisha usumbufu.

Shirika limesema watalaamu wao wanaendelea kufanyia kazi tatizo hilo na kwamba huduma kamili itarejea kuanzia saa 9:00 alasiri leo.

error: Content is protected !!