Mange amkana mbea wake

HomeBiashara

Mange amkana mbea wake

Mmiliki wa MangeKimambi App, Mange Kimambi amesema msichana aliyekamatwa na mke wa msanii Roma Mkatoliki sio mfanyakazi wake na hivyo kinachoendelea ni uigizaji tu.

Amesema hayo baada ya kuonekana video ikimuonyesha Mke wa Roma akimsema msichana mmoja ambaye bado jina lake halijafahamika kwamba kwanini alikua anamrekodi video ambayo imeenda kuwekwa kwenye programu tumizi (Application)  ya Mange Kimambi, na kusema kwamba mwanamke huyo anachepuka na mwanaume mwingine.

Mange ameweka video hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa Mke wa Roma anatafuta kiki kwani waliomkamata sio aliyetuma video na hivyo hamtambui.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Mange Kimambi (@mangekimambi_)

 

error: Content is protected !!