Pandora Leaks: Tambua njia wanazotumia viongozi wakubwa duniani kuiba mali

HomeKimataifa

Pandora Leaks: Tambua njia wanazotumia viongozi wakubwa duniani kuiba mali

Habari iliyopo duniani kwa sasa ni kuhusu ‘Pandora Leaks,’ ambazo ni nyaraka za siri zaidi ya mafaili milioni 12 ambayo yanaonesha mtandao wa fedha za viongozi wakubwa duniani kuanzia marais waliopo madarakani na waliopita, mawaziri, majaji na viongozi wengine wa ngazi za juu kabisa.

Lakini swali la wengi ni namna gani viongozi wanaweza kujilimbikizia mali, ambazo kwa kiasi kikubwa wamezikwapua kwa wizi kutoka kwenye Serikali zao.

Yapo maeneo hapa duniani ambayo viongozi wengi wa dunia hupenda kuficha mali zao, na maeneo haya yana sifa za kipekee kabisa ndio sababu ya kupendelewa zaidi kuendesha mitandao ya fedha haramu.

Ni maeneo gani hayo?

1. Andora 2. Bahamas 3. Belize 4. Bermuda 5. The British Virgin Islands 6. The Cayman Islands 7. The Channel Islands 8. Hong Kong 9. Monaco 10. Panama

Maeneo haya yana sifa gani?

1. Hakuna kodi kabisa ua ipo kwa kiwango kidogo sana. Hivyo ni sehemu nzuri kuwekeza fedha zako na zikazalisha zaidi.
2. Sehemu hizi zina ulinzi mkubwa sana wa taarifa binafsi za watu, na zinalindwa kwa sheria kabisa
3. Hakuna uwazi hata kidogo kwenye kufanya biashara huko
4. Hakuna kujenga kampuni, yaani huwezi kuwa na jengo la kampuni yako kwenye maeneo hayo.

Unaweza kufungua kampuni ya siri nje?
1. Anzisha kampuni kwenye moja ya maeneo hayo yenye usiri mkubwa wa taarifa.
2. Kampuni hiyo ipe jina tu, lakini isiwe na ofisi wala wafanyakazi
3. Inagharama kubwa kuanzisha, kwani sio mtu mwenye fedha ndio huanzisha, wapo wataalamu wa kazi hizo ambao wataanzisha kampuni kwa niaba yako.
4. Kampuni hizi zikishaanzisha kampuni hiyo watakutumia anuani za bodi ya wakurugenzi wote wa kampuni yako, majina tu, mtafanya kazi kwa uaminifu mkubwa, hii inafanywa kufuta ushahidi.

Ni kiasi gani cha fedha kimefichwa nje na viongozi wa dunia?
Bado haijajulikana rasmi ni kiasi gani, lakini umoja wa wanahabari wa (ICIJ) wanadai kuwa ni kati ya Dola trilioni 5 hadi dola trilioni 32. Benki ya Dunia inasema kuwa pesa zilizofichwa na viongozi kwenye maeneo hayo zinazigharimu Serikali zote duniani dola bilioni 600 kila mwaka kwenye upotevu wa mapato ya kodi.

error: Content is protected !!