Mpango: Tanzania inakopesheka

HomeKitaifa

Mpango: Tanzania inakopesheka

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema taasisi na mashirika makubwa duniani yameitaja Tanzania kama nchi moja wapo ambayo ipo kwenye nafasi nzuri ya kukopesheka.

Ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Jukwaa la Kodi na Uwekezaji 2024 akiwa kama mgeni rasmi.

“Taarifa za Mashirika makubwa duniani yanayopima uwezo wa nchi kukopesheka yameiweka Tanzania katika nafasi nzuri. Mathalani Taasisi ya Moody’s Investor Service imeipa Tanzania alama ya B2.” amesema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpangi ameongeza kwamba kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa za kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara, Tanzania imeendelea kuwa kitovu cha uwekezaji na nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi kusini mwa jangwa la Sahara licha ya misukosuko ya uchumi na kijamii inayoendelea duniani kote.

Aidha, Dkt. Mpango ametaja baadhi ya maboresho kama Kutoa vivutio vya kikodi ikiwemo kutoa misamaha ya kodi kwa kiwango cha 0% cha ushuru wa forodha, Kuendelea kufanya mashauriano baina ya Serikali na sekta binafsi kupitia baraza la taifa la biashara (TNBC), Kurekebisha sheria za kodi ili kutoa vivutio vya kodi kwa wakezaji na wafanyabiashara wa kimkakati na Kuweka utulivu wa sera za kodi ambapo viwango vya ushuru wa bidhaa vinafanyiwa marekebisho kila baada ya miaka mitatu badala ya kila mwaka.

error: Content is protected !!