Njia rahisi ya kupika chapati laini za kusukuma

HomeElimu

Njia rahisi ya kupika chapati laini za kusukuma

Chapati ni aina ya mkate ambao hauumuliwi kwa hamira. Chapati hutayarishwa kwa unga wa ngano na inahitaji umakini wakati wa kupika ili zisiwe ngumu na kuharibu utamu wake.

Mahitaji:

  • Unga wa ngano kilo 1 (kulingana na mahitaji)
  • Mayai 2
  • Chumvi
  • Maji
  • Siagi (butter) vijiko 3 vikubwa
  • Mafuta ya kula kwa ajili ya kuchomea
  • Iliki ya unga
  • Maziwa ya unga vijiko 3 vikubwa

Maelekezo:

  • Weka unga kwenye beseni au sufuria kavu kisha weka chumvi kiasi, maziwa vijiko 3 vya chakula na iliki kisha changanya mpaka uhakikishe vimechanganyikana vizuri.
  • Weka siagi vijiko vitatu kwenye unga kisha changanya hadi siagi ishikane na unga vizuri na iwe na uwiano mzuri (isionekane kabisa).
  • Pasua mayai pembeni, yakoroge vizuri na kisha weka kwenye unga. Changanya zaidi hadi upate uwiano unaofaa.
  • Ukiona uwiano mzuri wa unga wako, weka maji ya uvuguvugu kwenye unga na anza kukanda. Kanda unga mpaka uwe laini na haushikani na chombo unachokandia wala haunati kwenye mikono. Hapo unga utakua tayari.
  • Kata mabonge ya unga kwa umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo pembeni. Rudia hili zoezi hadi unga uishe.
  • Chukua donge moja moja, paka unga weka kwenye kibao cha kusumia chapati. Sukuma chapati hadi iwe sawa. Paka mafuta kwenye chapati na anza kukunja.
  • Rudia hilo zoezi kwa madonge yote yaliyobaki. Ukimaliza, anza kusukuma chapati zako kwa ajili ya kupika.
  • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri.
  • Weka chapati, acha iive hadi iwe rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili, paka mafuta upande uliokua wa kahawia. Geuza, paka mafuta tena upande mwingine.
  • Hakikisha chapati inaiva vizuri na inachambuka,hapo utakua umemaliza kazi na tayari kula chapati zako.
error: Content is protected !!