Fahamu sababu 8 zinazosababisha watu wasikupende

HomeElimu

Fahamu sababu 8 zinazosababisha watu wasikupende

Kuishi katika jamii inayokupenda hukufanya kuwa mwenye furaha na ufanisi katika yale unayoyafanya. Wapo baadhi ya watu wanatambua kuwa hawapendwi, lakini hawajui sababu za tatizo hilo wala njia ya kulitatua. Kama wewe ni mmoja wa wahanga na unahitaji kufahamu kwanini baadhi ya watu hawakupendi, basi hizi hapa sababu 8 zinazosababisha watu wasikupende.

1. Majivuno na majigambo
Mtu mwenye tabia ya majivuno na majigambo ni moja ya watu wanaochukiwa na kila mtu. Ikiwa unaleta majivuno ni dhahir kabisa hakika hutokuwa na rafiki bali utatengwa na watu katika jamii inayokuzunguka.

Tabia kama vile nina gari kali sana, mimi ndiye tajiri wa mtaa huu, nina akili sana, nina pesa usinione hivi, mambo yangu safi, wewe sio saizi yangu n.k. ni baadhi ya tabia mbaya za majivuno na majigambo.

Acha kujigamba na kujivuna katika jamii ili usiwe unatengwa na kuchukiwa.

2. Ubaguzi
Mtu mwenye ubaguzi huchukiwa na watu kwa kuwa anagawa watu kwa makundi. Haki ni msingi wa kuishi na watu vizuri, ikiwa una tabia ya kubagua watu kisa tu ni ndugu, marafiki, dini moja au kabila moja, basi acha tabia hiyo mara moja kwani itakufanya uchukiwe na watu.

3. Umbea na usengenyaji
Umbea na usengenyaji husababisha watu kugombana, kupigana, kuvunja familia na kuharibu maelewano katika jamii. Mtu mwenye tabia hizi anahitajika kuacha ili kurejesha upendo na mshikamano anaokosa kutoka kwa jamii, ndugu na jamaa. Epuka sana kuwa mbea na msengenyaji kwa kuwa unakuwa chanzo cha kupoteza amani na upendo katika jamii.

4. Lawama kwa wengine
Mtu anayependa kulaumu wengine katika jamii kutokana na mambo waliyoyafanya kwa pamoja kutokwenda sawa ni moja watu wasioelewekw katika jamii. Si busara kuwalaumu wengine hasaa kwa jambo mlilolifanya kwa pamoja pale inapotokea jambo hilo halijafanikiwabali ni vyema kutafuta suluhu pale mlipokwamia. Acha na pia punguza lawama kwa wezio na utaona mambo yakiwanyookea na upendo ukiongezeka.

5. Ubinafsi
Ubinafsi ni tabia mbaya ya kujijali wewe peke yako na mambo yako. Hakuna mtu atakayekupenda ikiwa wewe ni mtu unayejali tu mambo yako binafsi. Ni lazima wakati mwingine uthamini na kujali maisha na mambo ya watu wengine.

6. Uchoyo
Mtu anayetoa hupendwa katika jamii bila kujali anatoa kiasi gani. Kutoa haimaanishi utoe kupitiliza bali toa kile moyo wako unaridhia na unakuwa huru. Mfano kutoa rambirambi, kusaidia wasiojiweza kutakuweka karibu na jamii. Siyo lazima utoe mamilioni, kutoa hata soda moja au kumlipia mtu nauli ya daladala kuna maana kubwa.

Acha tabia ya uchoyo “Mchoyo hana rafiki.”

7. Ukorofi
Kama unavyopenda kusikilizwa, ndivyo ilivvo kwa watu wengine wanavyopenda kusikilizwa. Ikiwa huna muda wa kusikiliza mawazo au matatizo ya watu wengine, nao pia hawatakuwa na muda wa kupenda kukusikiliza.

Acha tabia za kulazimisha watu wakusikilize wewe nyakati zote, tambua nawe unapaswa kuwa na muda wa kuwasikiliza.

8. Uongo
Mtu mwongo ni hatari na unapokuwa na tabia ya kukanusha na kukataa mambo uliyoyatenda ilihali wewe ndio ulikuwa eneo la tukio hakuna mtu anaweza kupendezwa nawe zaidi utajijengea picha ya kutoaminika.

Kwa mfano unachukua kitu ukiulizwa unakana na kusema sio wewe, unakwenda mahali ukirudi ukiulizwa unakataa hukwenda n.k. Hakuna mtu atakayependezwa nawe kabisa zaidi unajijengea chuki.

Natumaini kupitia tabia tulizozianisha kuna jambo umejifunza na kama ni mmojapo kati ya  wneye tabia hizi badilika sasa uendane na jamii inayokuzunguka.

error: Content is protected !!