Wasifu wa Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani aliyejitoa leo kesi ya Mbowe

HomeKitaifa

Wasifu wa Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani aliyejitoa leo kesi ya Mbowe

Jaji Kiongozi Mustapha Siyani leo amekuwa jaji wa pili kujitoa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu kwa tuhuma mbalimbali za vitendo vya kigaidi.

Akitoa sababu ya kujiuluzu leo wakati kesi hiyo ikiendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi amesema ana majukumu mengine ambayo yanaweza yakamafanya akashindwa kuiendesha kesi hiyo haraka inavyotakiwa.

Siyani anakuwa jaji wa pili kujitoa kwenye kesi hiyo baada ya Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo awali kujitoa kufuatia watuhumiwa wote kumkataa.

Siyani ni nani?

Jaji Siyani alizaliwa Februari 25, 1977, Tunduru mkoani Ruvuma.

Alipata elimu ya msingi na sekondari katika wilaya za Tunduru na Songea kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Amesoma kidato cha tano na sita, Shule ya Songea Wavulana mwaka 1997 hadi 1999.

Alitunukiwa shahada ya sheria UDSM mwaka 2000 na kuajiriwa kama hakimu mkazi daraja la II, Mei 2005 mpaka Januari 2009.

     > Wasifu mfupi wa Jaji Luvanda aliyejitoa kesi ya Mbowe

Pia, alikuwa hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Mbarali,Mbeya Januari 2009 hadi Oktoba 2009.

Aliwahi kuajiriwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu kama ofisa utafiti. Alipata shahada ya uzamili (LLM) UDSM kati ya 2009 na 2010 akijikita kwenye masuala ya Katiba na Haki za Binadamu.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Siyani alikuwa naibu msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Alidumu katika nafasi hiyo kuanzia Februari 2015 hadi Aprili 15.

Aprili 15, 2018 aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Oktoba 8 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Jaji Siyani kuwa Jaji Kiongozi ambapo awali alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu. Aliteuliwa kushika wadhifa huo ulioachwa wazi na Eliezer Feleshi.

error: Content is protected !!