Nafasi za kazi 320 TAKUKURU

HomeKitaifa

Nafasi za kazi 320 TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetangaza nafasi 320 za kazi kwa vijana wa Kitanzania wenye umri usiozidi miaka 30.

Nafasi hizo zilizotangazwa kufuatia tangazo lililotolewa na Takukuru ni maofisa upelelezi nafasi 220 na nafasi 100 za wapelelezi wasaidizi daraja la tatu.

Tangazo hili limekuja ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Polisi kutangaza nafasi 500 za ajira na watu 50,000 kujitokeza kuwania nafasi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Takukuru leo Jumamosi, Januari 21, 2023, waombaji wa nafasi ya maofisa upelelezi wanatakiwa kuwa na Astashahada au shahada ya kwanza katika kozi ya uhandisi, usanifu, sayansi ya kompyuta, sheria na saikolojia.

error: Content is protected !!