Rwanda kugawa simu bure kwa Wananchi

HomeKimataifa

Rwanda kugawa simu bure kwa Wananchi

Serikali ya Nchi ya Rwanda inatarajia kusambaza simu za kisasa takribani 14,000 kwa wananchi wake kwenye kampeni inayojulikana kama “Connect Rwanda Challenge”, Kampeni hiyo ilizinduliwa 2019 kwa watu binafsi na taasisi kuhamasishwa kuchangia kwa kutoa simu za kisasa kwa wananchi wasio na uwezo wa kuzinunua.

Kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Uviko 19 kampeni hiyo ilisimama ila inatarajiwa kuanza tena Novemba 15 mwaka huu, Takribani simu 7650 za kisasa zimesambazwa kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu nchini Rwanda.

  > Ukatili kwa waandishi wa habari wapungua

Zaidi ya wanawake wakulima 3,000 wanatarajia kunufaika na ugawaji huo wa simu za kisasa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa nchi hiyo kuziba pengo la changamoto za jinsia katika matumizi ya simu za mkononi katika sekta ya kilimo ambayo 60% ya wakulima ni wanawake.

Kupitia simu hizo wakulima wa nchini Rwanda watanufaika kwa kuweza kufikiwa na wataalamu wa kilimo kupitia simu hizo za kisasa, Wakulima watapata taarifa za kilimo kwa urahisi na kusaidia ongezeko la uzalishaji.

error: Content is protected !!