Masharti 7 ya Samia Scholarship

HomeElimu

Masharti 7 ya Samia Scholarship

Serikali imetangaza masharti saba kwa wanafunzi watakaoomba kunufaika na ufadhili (Samia Scholarship), ikiwemo kuhakikisha kuwa kiwango cha ufaulu hakishuki chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo baada ya kupewa ufadhili huo.

Masharti mengine ni mnufaika kutoruhusiwa kuahirisha masomo isipokuwa kwa sababu za kiafya, kuthibitishwa na chuo husika, kuwa na akaunti ya benki kwa ajili ya kuingiziwa fedha, kusoma na kuelewa mkataba wa makubaliano ya ufadhili wa amsomo kati yake na Wizara ya Elimu kabla ya kusaini na mnufaika kujisajili katika mfumo wa usimamizi wa wanafunzi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema ufadhili huo utahusisha ada ya mafunzo, posho ya chakula, malazi, vitabu, mahitaji maalumu ya vitivo, vifaa saidizi kwa wenye mahitaji maalumu na bima ya afya.

Alisema majina ya wanafunzi waliopata ufaulu wa juu kwenye masomo ya Sayansi katika mitihani ya kidato cha sita, yalianza kutangazwa jana katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB).

“Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa.” alisema Waziri Mkenda.

error: Content is protected !!