Bashungwa asimamisha kazi watano Manyara

HomeKitaifa

Bashungwa asimamisha kazi watano Manyara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa amewasimamisha kazi Maafisa watano Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Halmashauri hasara.

Watumishi hao ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Juma Ibarahim Mavumo; aliyekuwa Kaimu mweka hazina, Ramadhani Mwakamyanda; Mweka hazina wa sasa, Respicius Kagaruki; Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Nyanda Komanya Msirikale na Mhasibu wa Mapato, David Assey.

Amechukua hatua hiyo Septemba 27, 2020 wakati akifanya majumuisho ya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ na Halmashauri ya Mji Mbulu, mkoani Manyara.

Bashungwa amesema mnamo tarehe 12 Julai 2022 aliyekuwa anakaimu ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbulu, Ndugu David Ali Assey aliandika barua kwa Kampuni binafsi ya kukopa kiasi cha Sh milioni 6.7 kwa aijli ya matumizi ya ofisi na kuelekeza fedha hiyo kuwekwa kwenye akaunti binafsi ya Davidi ali Assey ambaye ni Mhasibu wa Halmashauri.

error: Content is protected !!