Rais Samia: Tunakwenda kuandika historia Kigoma

HomeKitaifa

Rais Samia: Tunakwenda kuandika historia Kigoma

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Mkoa wa Kigoma leo unaandika historia kwa kuzimwa kwa majenereta yaliyokuwa yakizalisha umeme na sasa unaunganishwa kwenye gridi ya taifa.

Aidha, ameagiza uwekezaji uanze mkoani humo kwa kuwa uko katika eneo lililozungukwa na nchi zenye fursa.

Rais Samia aliyasema hayo jana jioni wilayani Kibondo kwenye mkutano wa hadhara akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara ya siku nne mkoani humo.

“Tunakwenda kuandika historia kwa Kigoma kuunganishwa kwenye umeme wa gridi na majenereta mwisho kesho (leo) , nitakwenda kuyazima, umeme utakuwa mwingi, tunaifungua Kigoma kibiashara, lakini pia umeme huo tuliingia makubaliano na majirani zetu kuwapelekea,” alisema Rais Samia.

Alihimiza wananchi wa Kigoma na maeneo mengine waendelee kuishi kwa amani, utulivu na mshikamano huku kila mmoja akifanya kazi kwa bidii katika eneo lake ili serikali iendelee kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo.

“Kama ni mkulima lima kwa bidii, kila mmoja achape kazi katika eneo lake, maendeleo hayaji kwa muujiza, serikali sisi viongozi wenu tunafanya kazi ni kazi, kazi, kazi,” alisema Rais Samia.

 

error: Content is protected !!