Squid Game kufungiwa Kenya

HomeBurudani

Squid Game kufungiwa Kenya

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Uainishaji nchini Kenya (KFCB), Christopher Wambula amewashauri wazazi kuwa waangalifu na kufuatilia video ambazo watoto wao hutazama na kuwakataza kuangalia filamu ya Squid Game kwenye mtandao wa Netflix.

Wambula alisema hayo kutokana na maudhui yaliyomo ndani ya filamu hiyo kwamba hayana mafunzo mazuri kwa watoto pia amesema hata Netflix wenyewe wameweka angalizo kwamba itazamwe na watu walio juu ya miaka 18 tu ili kuepuka na matatizo yanayojitokeza baada ya watoto kutazama filamu za aina hiyo.

> Movie hii itanogesha siku yako

“Ikumbukwe kwamba mwaka 2021, kijana mmoja huku Kenya aliripotiwa akikiri kwamba aliwaua wazazi wake pamoja na ndugu zake kutokana na ushawishi aliopata baada kuangalia filamu ya ‘Killing Eve’,” alisema Wambula.

Squid Game iliachiwa rasmi 17 Septemba mwaka na kushika nafasi ya kwanza kwenye nchi 90 ndani ya siku 10.

error: Content is protected !!