Movie hii itanogesha wikiendi yako

HomeBurudani

Movie hii itanogesha wikiendi yako

Wikiendi  watu hupenda kutoka kwenda sehemu mbalimbali kufurahi na ndugu, jamaa, marafiki au wapenzi wao lakini kwa wewe ambaye hupendi kutoka basi hakijaharibika kitu kwani unaweza kubaki na kutazama filamu itakayo kuburudisha, na hii sio nyingine bali ni SQUID GAME.

Ni filamu yenye visa na mikasa mbalimbali inayohusu maisha ya kila siku huku dhamira kubwa ikiwa kuonesha jinsi watu maskini wanavyojitoa ilikuweza kupata fedha za kujikimu na kulipa madeni.

Kiasi kikubwa cha fedha  kinawekwa ili washiriki waweze kucheza mchezo na mshindi kuondoka na pesa hizo. Katika mashindano hayo ndipo mauaji, uonevu pamoja na visa vingine vyakufurahisha na kuhuzunisha vinatokea.

Hivyo basi kwa wapenzi wa filamu basi weekend yako itakuwa nzuri sana kama utatenga muda wako kutazama filamu hii.

error: Content is protected !!