Hapatoshi Ruby na Saraphina

HomeBurudani

Hapatoshi Ruby na Saraphina

Mwanamuziki wa kike anaekuja kwa kasi katika tasnia ya Bongo Fleva anaejulikana kama Saraphina, amefunguka kuhusu msanii mwenzake Ruby kushindwa kuonyesha ushirikiano kwenye nyimbo  ambayo waliimba pamoja.

Hivi karibuni Saraphina alitoa wimbo unaojulikana kama “ Number One” ambao amemshirikisha Ruby, Katika moja ya mahojiano na kipindi cha redio Saraphina aliulizwa inakuaje Ruby hatoi ushirikiano kwenye kuutangaza wimbo huo?Saraphina alijibu kwa kusema kwasababu ile ni nyimbo yake basi yeye ana jukumu la kuutangaza huo wimbo ila ikitokea mtu mwingine anataka kuutangaza sawa hawezi kumzuia.

Ila hajui ni nini kimetokea lakini Ruby alifuta mpaka picha katika ukurasa wake wa Instagram ambazo alikua yuko na Saraphina.

Ruby ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao mara nyingi wanatuhumiwa kuwa na jeuri lakini kwa upande wake yeye anasema si ujeuri ila ni misimamo, aidha kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika kupiti Insta Story yake kuwa,

“Hivi mtu unamuombaje msanii aje kufanya show alafu akikupa bei yake unamjibu wasanii tunao wengi, vitu vingine bana! sa siuwafwate hao wengi” alianndika Ruby nakuweka maneno ya kusindikiza kwa kusema msipende kudharau kazi za watu imetosha.

error: Content is protected !!