Polisi adakwa akivuta bangi

HomeKimataifa

Polisi adakwa akivuta bangi

Inspekta Jenerali wa Polisi jijini Lagos, Usman Baba Alkali ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa lengo la kufichua utambulisho wa afisa wa polisi aliyekamatwa akivuta bangi hadharani muda wa kazi. 

Agizo hilo limekuja baada ya kusambaa kwa picha za afisa aliyevalia mavazi kamili ya polisi akiwa amekaa na mkononi ameshika msokoto mmoja wa bangi aliokuwa akivuta.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Afisa Uhusiano wa Kikosi cha Usalama Barabarani, CSP Muyiwa Adejobi, alilaani tukio hilo.

Alitoa hakikisho kuwa IGP atahakikisha anachukuliwa hatua zinazohitajika za kinidhamu dhidi ya polisi huyo kwa kitendo chake cha aibu.

“Hii inalaaniwa kwa ujumla wake. Ni bahati mbaya sana kwamba tunaweza kuona afisa wa polisi, aliyevaa sare, akishuka hadi kiwango hiki. Tunapinga hii ili kutumika kama kizuizi kwa wengine.” alisema IGP. 

 

error: Content is protected !!