Historia ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais Afrika

HomeMakala

Historia ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais Afrika

Kuna wanawake waliowahi kuwa Marais Afrika kabla ya mwaka 2006. Hao ni pamoja na Slyvie Kiningi aliyerithi kiti cha Urais nchini Burundi (Februari-Oktoba 1993) kufuatia kuuwawa kwa aliyekuwa Rais (Melchior Ndadaye) na Ivy Matsepe-Cassaburi aliyeteuliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwa kipindi cha wiki mbili mwaka 2005 kufuatia kujiuzulu kwa Thabo Mbeki.

Lakini mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais barani Afrika, ni Ellen Jonson Sirleaf wa Liberia.

Ellen Johson Sirleaf ni nani?

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1938 katika mji wa Monrovia huko Liberia.

Alisoma katika shule za nchini mwao kabla ya kwenda Marekani alikosoma katika Chuo cha Biashara cha Madison na Chuo Kikuu  cha Harvard.

Alirudi Liberia mwaka 1971 ambapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha kabla ya kuondoka tena nchini mwao mwaka 1974 na kwenda kufanya kazi Benki ya Dunia.

Mwaka 1979, Ellen Jonson Sirleaf alirudi tena Liberia na kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, nafasi ambayo alidumu nayo kwa mwaka mmoja tu.

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchi Liberia mwaka 1980, Sirleaf aliondoka tena Liberia na kurudi Marekani.

Mbio za kuingia Ikulu

Mwaka 1985, Sirleaf alijitokeza majukwaani akitaka kuwa Makamu wa Rais, lakini mwaka huo huo alikamatwa na kuhukumiwa miaka 10 jela baada ya hotuba yake iliyomponda vikali Samuel Doe aliyekuwa Rais.

Hata hivyo kutokana na shinikizo kubwa kwa Serikali lilitoka nje na ndani ya Liberia, Sirleaf aliachiwa huru lakini aliondolewa kwenye nafasi aliyokuwa akigombea. Badala yake aligombea nafasi ya Useneta katika jimbo la Montserrado. Licha ya kwamba alishinda kiti hicho, Sirleaf aligomea ushindi na kuungana na wengi walioupinga uchaguzi huo.

Mwaka 1997. Sirleaf aligombea Urais na kupata asilimia 25 ya kura huku mpinzani wake Charles Taylor akipata ushindi kwa asilimia 75.

Baada ya utata uliobuka katika kupinga matokeo hayo, Bi Sirleaf alipewa mashtaka ya uhaini, akalazimika kwenda kuishi uhamishoni nchini Ivory Coast.

Urais

Mwaka 2005 Sirleaf alijtosa kugombea Urais akichuana na gwiji wa soka na Rais wa sasa wa Liberia, George Weah. Bi Ellen Jonson alishinda kwa asilimia 59 ya kura na kuandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais barani Afrika.

Mwaka 2011 alishinda tena Urais, akadumu hadi 2018 alipoachia kiti hicho kidemokrasia, na kurithiwa na George Weah.

Ellen Johson Sirleaf alishinda tuzo ya Nobel mwaka 2011 kufuatia mchango wake katika kuongeza wigo wa wanawake kushiriki kwenye kupigania amani.

 

error: Content is protected !!