Ajifanya Makamu wa Rais na kutibiwa bure

HomeKimataifa

Ajifanya Makamu wa Rais na kutibiwa bure

Hii nayo kali : jamaa mmoja kafika zake hospitali, akajitambulisha kama Makamu Rais, akapewa heshima zote na kupatiwa matibabu bure kabisa.

Imetokea huko nchini Zimbabwe mwezi uliopita ambapo Marlon Katiyo (35), alitembelea hospitali mbili mara kadhaa na kujitambulisha kama Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Constantino Chiwenga. Matatibu wakampatia matibabu ya maumivu ya kichwa kwa heshima zote wakidhani wanamhudumia Makamu wa Rais.

Badaae Bwana Katiyo alishtukiwa, amepelekwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya ulaghai. Bwana Katiyo amekata rufaa, na sasa watu wengi wa Harare na maeneo mengine ya Zimbabwe wanasubiri kusikia maamuzi ya hakimu Dennis Mangosi aliyekabidhiwa kesi hiyo.

error: Content is protected !!