Serikali kuongeza mapato kupitia Facebook, Twitter na Google

HomeUncategorized

Serikali kuongeza mapato kupitia Facebook, Twitter na Google

Hivi karibuni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alisema kuwa Serikali ya Tanzania inatafuta namna ya kuyabana makampuni makubwa ya mitandao kama Google, Facebook na Twitter yalipe kodi nchini.

Baada ya taarifa hiyo ya serikali, kumekuwa na maswali mengi, na miongoni mwa hayo, wengi wameendelea kujiuliza kama inawezekana kufanya hivyo au la.

Hii inawezakana kabisa kwa kutazama mataifa mengine yanafanyaje. Kampuni tanzu ya Facebook, Whatsapp, imepigwa faini ya dola za kimarekani milioni $266 (shilingi bilioni 616.8) kwa makosa ya kushindwa kuweka wazi matumizi ya taarifa inayokusanya kwa watumiaji kutoka nchi ya Umoja wa Ulaya (EU).

Hii ni faini ya pili kwa ukubwa kwa kampuni za kimarekani ndani ya Umoja wa Ulaya. Whatsapp imekuwa ikukusanya taarifa za watu kwenye simu zao na kusambaza taarifa hizo kwa kampuni mama ya Facebook bila ruhusa ya watumiaji wa mitandao hiyo.

EU imetoa miezi mitatu kwa Facebook kuhakikisha wanarekebisha sheria zake za faragha za watumiaji kuendana na sheria zao.

Msemaji wa Whatsapp amesema hawakubaliani na maamuzi hayo, na wanakusudia kukata rufaa, kwani tangu 2018 wamehakikisha wanafanya kazi kwa weledi, uwazi na kutii sheria za kila nchi.

Kwa mazingira hayo, ni wazi kabisa kuwa hata Tanzania inaweza kutoa matakwa na masharti yake kwa kampuni hizo kubwa ili kufanya kazi zake hapa nchini. Huduma za malipo zinahamia mitandaoni kwa kasi sana, kama taifa ni lazima litafute namna ya kwenda na kasi ya dunia kwa maendeleo ya yetu.

error: Content is protected !!