New Zealand: Mwanamke afariki muda mfupi baada ya kuchanjwa chanjo ya Pfizer

HomeKitaifa

New Zealand: Mwanamke afariki muda mfupi baada ya kuchanjwa chanjo ya Pfizer

Nchi ya New Zealand imeripoti kifo cha kwanza ambacho kinahusishwa moja kwa moja na chanjo ya Pfizer.

Bodi huru ya kufuatilia usalama wa chanjo nchini New Zealand imesema kuwa kifo cha mwanamke huyo pengine kimetokana na “myocarditis” (Tatizo la misuli ya moyo kupata joto kali na moyo kushindwa kusukuma damu vizuri).

Wataalamu wa tiba Ulaya wamesema kuwa, tatizo hilo la “myocarditis” ni adimu sana kwa watu hivyo haifanyi chanjo kutokuwa salama. Sababu hasa za kifo cha mwanamke huyo bado hazijawekwa wazi, lakini bodi huru ya usalama wa chanjo imeshikilia msimamo wake kwa kusema kuwa kifo cha mwanamke huyo kimesababishwa na chanjo ya Pfizer.

Hiki ni kifo cha kwanza kabisa kuripotiwa nchini New Zealand baada ya mtu kupigwa chanjo ya Pfizer. Sababu za kifo bado zinachunguzwa, na mamlaka husika bado hazijatoka taarifa kuhusu mwanamke huyo.

Idara ya Dawa Ulaya imesema kuwa hali ya moyo kupata joto kali kweli ipo, hasa kwa chanjo za Moderna na Pfizer, lakini hali hii ni adimu sana na hutokea kwa watu wenye umri mdogo.

Dalili za “myocarditis” ni maumivu makali ya kifua, kushindwa kupumua vizuri na mapigo ya moyo yasiyokuwa ya kawaida.

Ukipata dalili hizo baada ya kupigwa chanjo, tafadhali muone daktari.

error: Content is protected !!