Mtoto auawa na kutolewa sehemu za siri

HomeKitaifa

Mtoto auawa na kutolewa sehemu za siri

Mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Tutuo, wilayani Sokonge , Mkoa wa Tabora, Maria Ngassa(13) ameuawa kikatili wakati akienda kisimani na watu wasiojulikana  kisha kutolewa sehemu zake za siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa polisi wanachunguza kubaini chanzo cha mauaji hayo na wauaji waliohusika.

Baba mzazi wa Maria anayefahamika kama Ngassa Kazungu anaeleza kwamba kabla ya mwanaye kuuawa alimtuma akachote maji kisimani, hivyo akaenda na kurudi lakini alipokwenda kwa mara ya pili hakurudi na mwili wake uliokotwa kichakani siku iliyofuata ukiwa umenyofolewa sehemu za siri na pia masikio yametobolewa na kitu chenye ncha kali.

“Jamani wananchi mwenzenu nimepata pigo kubwa sana ambalo sitalisahau katika maisha yangu, mtoto wangu Maria ameuawa kikatili sana , niliamua kumsomesha mwanangu ili siku za mbeleni aje kunisaidia lakini wameamua kukatiza maisha yake laah, naumia sana,” alisema Kazungu huku akilia.

 

error: Content is protected !!