Shaka ajibu mapigo ya NCCR-Mageuzi

HomeKitaifa

Shaka ajibu mapigo ya NCCR-Mageuzi

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amejibu tuhuma zilizotolewa na mwanasiasa Joseph Selasini kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewahi kumtumia James Mbatia au kuwa na ushirikiano na NCCR-Mageuzi.

Shaka alisema chama kimesikitishwa na madai hayo ya upotoshaji unaotaka kuihusisha CCM katika sakata linalotoka ndani ya NCCR-Mageuzi.

“Kinachofanywa  na Selasini  ni kujitafutia  umaarufu wa bei  chee na kutaka kuipaka matope CCM kwa ajenda ambayo tokea kuasisiwa kwa chama chao imekuwa ndio muelekeo wao katika maisha yao ya  siasa,

“wa kuwasaidia,CCM tunamshauri Selasini na wanasiasa aina yake kujipanga kimkakati kuimarisha vyama vyao ikiwemo kuboresha na kuziishi katiba zao ili kuondokana na migogoro ya madaraka hali inayozorotesha demokrasia ndani ya vyama vyao,” alisema Shaka.

Aidha, Shaka alisema kwamba kwa sasa ajenda kubwa ya CCM ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuhuisha demokrasia nchini.

“Kwa  wakati huu CCM kama chama kiongozi na mlezi wa siasa nchini  tunalo jukumu moja tu, la kumuunga mkono Rais Samia  Suluhu Hassan katika safari ya maridhiano aliyoianzisha hivyo hatuwezi kurudi nyuma bali kusonga mbele” alisema Shaka.

Hivi karibuni, Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi iliwasimamisha kujihusisha na shughuli zozote ndani ya chama mwenyekiti, Mbatia na sekretarieti yake hatua iliyopingwa na Mbatia.

error: Content is protected !!