Rais Samia aridhia Balozi Mulamula kugombea Ukatibu Mkuu

HomeKitaifa

Rais Samia aridhia Balozi Mulamula kugombea Ukatibu Mkuu

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Balozi Liberata Mulamula kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola akiamini kuwa kutokana na uzoefu wake mkubwa katika masuala ya diplomasia atakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa Tanzania na jumuiya hiyo.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuchaguliwa kwa Balozi Mulamula ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki kutakuwa na manufaa makubwa kwa kuwa atasaidia baadhi ya ajenda za Tanzania kuzingatiwa ndani ya jumuiya.

“Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imepitisha jina lake na inamuunga mkono kwa sababu inaamini juu ya uwezo wake, ataiwakilisha nchi vizuri, atakuwa balozi mzuri kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema.

Msigwa aliwaomba wajumbe watakaohusika katika kumpitisha Balozi Mulamula kumpa kura za kutosha kwa sababu atatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla.

error: Content is protected !!