Spika apiga marufuku vituko bungeni

HomeKitaifa

Spika apiga marufuku vituko bungeni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Tulia Ackson amepiga marufuku Wabunge kufanya vituko kama kupiga magoti au sarakasi wakati wakichangia mijadala mbalimbali ndani ya Bunge.

Dr. Tulia ametoa maelekezo hayo baada ya Mbunge wa Igalula, Venant Daud Protas kuomba mwongozo wa Spika akitaka kujua kama Bunge linaruhusu Wabunge kuchangia mijadala kwa kufanya vituko ndani ya bunge.

Mbunge Daud Protas ameomba muongozo huo kufuatia mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Gregory Massay kupanda juu ya meza na kupiga sarakasi wakati akichangia mjadala ndani ya bunge juzi Mei 23, 2022, tukio jingine limefanywa na Mbunge wa viti Maalumu, Jacqueline Ngonyani Msongozi ambaye amepiga magoti wakati akiwasilisha hoja yake jana Mei 24,2022.

 

error: Content is protected !!