Bweni la Bwiru Boys lateketea

HomeKitaifa

Bweni la Bwiru Boys lateketea

Zaidi ya wanafunzi 70 katika shule ya wavulana ya Bwiru sekondari iliyopo manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamenusurika kifo baada ya bweni kuteketea kwa moto. Tukio hilo limetokea majira ya saa 3:40 usiku wa kuamkia leo wakati wakiwa madarasani wakijisomea masomo yao ya ziada.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Eng. Robert Gabriel amesema, serikali ya mkoa huo itahakikisha wanafunzi shule ya sekondari Bwiru ambayo moja ya bweni limeungua moto usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2022 wanapatiwa vifaa vyote vilivyoteketea katika tukio hilo ili waweze kuendelea na masomo.

error: Content is protected !!