Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 08 (Lampard na Gerrad kuchukua mikoba ya Bruce kunako Newcastle, Asensio kujiunga na Liverpool)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 08 (Lampard na Gerrad kuchukua mikoba ya Bruce kunako Newcastle, Asensio kujiunga na Liverpool)

Wamiliki wapya wa Newcastle wanalenga kuifanya klabu yao iwe kubwa kama Manchester City na Paris St-Germain kiushindani (Times).

Kocha wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard na kocha wa Rangers, Steven Gerrard wanatazamiwao kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa Newcastle Steve Bruce, ambaye amesema anatarajia kupoteza kazi yake (Telegraph).

Manchester City wameonyesha nia ya kufungua mazungumzo ya mkataba na Raheem Sterling 26, inasemekana hawataki kumuuza mchezaji huyo, ambaye amebakiza mkataba usiozidi miaka miwili (Sun).

Klabu ya Barcelona imekuwa ikihusishwa sana na Sterling ambapo Manchester City nao wamehushishwa kuhitaji huduma ya winga wa Ufaransa Ousmane Dembele 24, kama mbadala ikiwa mchezaji wao angehamia Camp Nou (El Nacional).

Manchester United na Chelsea zinamlenga mshambuliaji wa Stoke City wa Uingereza Emre Tezgel 16. Manchester City pia inasemekana inamnyatia kijana huyo (Star).

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi (26) ameripotiwa kupokea ofa kutoka Barcelona katika usajili wa dirisha dogo Januari. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji unaisha mwisho wa msimu huu, mchezaji huyo pia amekuwa na wakati mgumu kupata namba kikosi cha kwanza chini ya kocha Jurgen Klopp (Sun).

Liverpool inaagalia uwezekano wa kumsajili winga wa Real Madrid Marco Asensio 25, ambaye anaripotiwa hana furaha pale Bernabeu (Mirror).

Klabu ya Juventus ipo tayari kumuuza kiungo wake Weston McKennie (23) kwa dau la pauni milioni 24.5, mchezaji huyo anahusishwa na mazungumzo na klabu ya Tottenham Hotspurs (Calcio Mercato – Italian)

Kiungo wa England Harry Winks 25, anahusihwa kujiunga na klabu ya Everton akitokea Tottenham ifikapo Januari ili kupata nafasi ya kucheza (Caught Offside)

Juventus na Inter wapo katika mbio za kumsajili beki wa pembeni wa Leicester City Timothy Castagne, 25 (Le Derniere Heure).

AC Milan imeonyesha nia ya kumsajili beki wa Ufaransa Samuel Umtiti 27, kutoka Barcelona dirisha dogo la usajili Januari (Calcio Mercato – Italian).

Mshambuliaji wa Torino na Italia Andrea Belotti 27, anaweza kuondoka klabuni hapo bure mkataba wake utakapokwisha mwisho wa msimu huu (Fabrizio Romano).

Mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic 21, anayekipiga kunako klabu ya Fiorentina na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mauro Icardi (28) wapo kwenye orodha ya wachezaji wanaohitajika na klabu ya Juventus (Gazzetta dello sport – Italian).

error: Content is protected !!