500,000 ikifichua wezi miundombinu ya umeme

HomeKitaifa

500,000 ikifichua wezi miundombinu ya umeme

Shirika la Umeme Nchini  (TANESCO), limetangaza zawadi ya sh. 500,000 kwa mwananchi atakayefichua wezi wa miundimbinu ya umeme.

Shirika hilo limesema lengo la kutoa fedha hiyo ni kuhakikisha miradi ya TANESCO inalindwa na kuwanufaisha wananchi na ikibainika katika maeneo yao kumehujumiwa miundombinu, serikali iitaanza kuchukua hatua kwa kamanda wajadi (sungusungu).

Ofisa Usalama Kanda ya Magharibi wa TANESCO, Saidi Songwe alibainisha hayo jana kwenye kikao cha kushirikisha jeshi la jadi (sungusungu) kutoka kata 58 za wilayani Kahama mkoani Shinyanga kulinda miundombinu ya shirika.

“Serikali inatoa fedha nyingi katika kusogeza huduma ya nishati kwa wananchi, baadhi yao wanaihujumu kwa kuiba nyaya za kopa na mafuta kwenye transfoma mabazo zinasaidia kulinda uhai wa transfoma na kufanya kazi vyema,” alisema Songwe.

Aidha, Mwenyekiti wa Sungusungu wilaya, Muzari Kashindwa alisema atahakikisha anafanya mikutano ya mara kwa mara kulikumbusha wajibu jeshi lake lajadi ikiwamo kulinda miundombinu. 

 

 

 

error: Content is protected !!