Marufuku kusafirisha wanyamapori

HomeKitaifa

Marufuku kusafirisha wanyamapori

Waziri wa Maliasi na Utalii Pindi Chana ameagiza kusitishwa mara moja kwa usafirishaji wa wanyamapori nje ya nchi kama ambavyo ilitangazwa juzi na Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania.

“Toka jana [juzi] kuna taarifa iliyokuwa inasambaa kuhusu tangazo la usafirishaji wa wanyamapori nje ya nchi, kama Waziri mwenye dhamana nachukua nafasi hii kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori hao mpaka Serikali itakapopata taarifa rasmi kutoka katika Taasisi husika na Serikali kuamua vinginevyo”

“Kwa maelezo yangu haya, hakuna tena usafirishaji wa wanyamapori hao kama ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo Taasisi”

Itakumbukwa jana[juzi] ilitolewa taarifa kuhusu usafirishaji wa Wanyamapori hai nje ya nchi kwa Wafanyabiashara waliokuwa na Wanyamapori wakati zuio la Serikali la kusafirisha Wanyamapori hai nje ya nchi la mwaka 2016 ambapo taarifa ilisema ruhusa hiyo haihusu wanyamapori wakubwa wala haihusu ukamataji mpya porini, bali inahusu wanyapori wale tu ambao wananchi walikuwa nao kwenye mashamba yao ya ufugaji kama vile kobe, jongoo.

error: Content is protected !!