Ugonjwa mpya Tanzania

HomeKitaifa

Ugonjwa mpya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekiri kuwepo kwa ugonjwa usiofahamika ambao husababisha watu kutokwa damu puani na kisha kuanguka.

Akizungumza na viongozi wa dini katika Mkutano Mkuu wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA), Rais Samia alitaja mikoa ya kusini mwa Tanzania kuwa sehemu ambapo ugonjwa huo upo.

“Nilikuwa nazungumza na waziri mkuu juzi, ametoka ziara kule mikoa ya kusini, Lindi ananiambia ameona kuna maradhi yameingia, wanadamu wanatokwa tu na damu za pua na wanadondoka”, 

Hatujui ni kitu gani ila Wanasayansi na Wataalamu wa Afya wote wamehamia huko wanaangalia ni kitu gani?, kwanini Mwanadamu atokwe tu na damu za pua adondoke, angekuwa mmoja wawili tungesema Presha imepanda vein zimepasuka anatokwa damu za pua lakini ni wengi kwa mfululizo ni maradhi ambayo hatujawahi kuona” alisema Rais Samia.

Mkutano huo wa AMECEA, shirikisho linaloundwa na nchi 8 ambazo ni Zambia, Malawi, Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia, Eritrea na mwenyeji Tanzania, ambapo pamoja na mambo mengine umejiegemeza kwenye masuala ya utunzaji wa mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu ya binadamu.

error: Content is protected !!