Pacha mmoja afariki

HomeKitaifa

Pacha mmoja afariki

Pacha mmoja kati ya waliotenganishwa  Julai Mosi mwaka huu (Rehema na Neema) katika Hospitali ya Muhimbili amefariki dunia baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Aminiel Elgaesha, Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kutokea kwa kifo cha Neema licha ya mapacha hao kufanikiwa kuvuka saa 72 za uangalizi wakiwa ICU.

“Ilipofika Jumapili saa tatu asubuhi mtoto mmoja ambaye ni Neema hali yake ilibadilika ghafla na madaktari wakaendelea kujitahidi kuona namna ambavyo wanaweza wakamrudisha katika hali yake ya kawaida lakini ilishindikana”amesema Elgaesha.

Aidha, mtoto Rehema aliyebaki anaendelea vizuri na madaktari wanaendelea kutoa huduma sahihi na kwa wakati.

 

error: Content is protected !!