Rais Samia ahimiza sheria zitafsiriwe kwa Kiswahili

HomeKitaifa

Rais Samia ahimiza sheria zitafsiriwe kwa Kiswahili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inahitaji sheria madhubuti kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na umiliki wa rasilimali.

Rais Samia amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (Women in Law and Development in Africa- WiLDAF) yaliyofanyika ukumbi wa Serena.

Aidha, Rais Samia amesema licha ya takwimu kuoneysha kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji, bado baadhi ya mila na desturi zinawafanya wanawake kuendelea kukandamizwa.

Rais Samia amesema Sheria ni nyenzo kuu ya ufikiwaji na usawa wa kijinsia na ustawi wa wanawake hivyo kutoa kipaumbele kwa wanawake ni jambo la lazima ili kuleta maendeleo.

Pia, Rais Samia amesema ipo haja ya kufanya tathmini ya Sheria zilizopo na kuona zina mchango gani kwa Watanzania na kuhakikisha kuwa zinakwenda ngazi za chini ili ziweze kutambuliwa na kufahamika kwa wananchi.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa Sheria kutungwa na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kurahisisha kutoa elimu na ufahamu kwa wananchi.

error: Content is protected !!