Rais Samia atengua zuio la mikutano ya hadhara

HomeKitaifa

Rais Samia atengua zuio la mikutano ya hadhara

Rais Samia Suluhu Hassan ameruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iliyozuiliwa kwa muda huku akiwataka wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu na kuzingatia sheria na kununi wakati wakiendesha shughuli zao.

“Mikutano ya hadhara ni haki ya vyama vya siasa, nimetoa ruhusa ya kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa lakini tuna wajibu, Serikali tumeshajipanga kwa wajibu wetu, wajibu wetu ni kulinda mikutano ya vyama vya siasa.

“Wajibu wenu vyama vya siasa ni kufuata sheria na kanuni zinavyosema lakini kama waungwana wastaarabu niombe sana tunatoa ruhusa ya vyama vya siasa twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, kafanyeni siasa za kupevuka, siasa za kujenga na si kubomoa na kurudi nyuma tulikotoka,” amesisitiza Rais leo Januari 3, 2022 alipokutana na viongozi wa vyama 19 venye usajili kamili wa siasa nchini

 

 

error: Content is protected !!