Sharubati (Juice) za Ceres zakutwa na sumu

HomeKimataifa

Sharubati (Juice) za Ceres zakutwa na sumu

Kampuni kutoka Afrika Kusini inayotengeneza sharubati aina ya Ceres imerudisha kiwandani baadhi ya bidhaa hizo zilizosambazwa kwenye nchi saba kutokana na kukutwa na kiwango kikubwa cha kemikali aina ya Patulin.

Patulin ni viambata vya sumu (mycotoxin) ambavyo huzalishwa na aina fulani ya fangasi ambao hukaa kwenye bidhaa za vyakula. Viambata hivyo hutokea kwenye chakula kama ishara ya athari za fangasi kwenye mazao kabla na baada ya kuvunwa.

> Madhara 8 makubwa yatokanayo na unywaji soda

Watumiaji kutoka Kenya, Zambia, Zimbabwe, Uganda, Mauritius, Shelisheli na Congo wamepewa tahadhari, na kutakiwa kurudisha bidhaa za toleo kuanzia Juni 14 mpaka 30, 2021.

Uamuzi huo umekuja baada ya majibu kutoka maabara kuonesha kuwa kiwango cha Patulin katika sharubati hizo kuvuka kiwango cha kawaida kilichopitishwa na sheria.

error: Content is protected !!