Chalinze yapokea gari la Zimamoto na Uokoaji

HomeKitaifa

Chalinze yapokea gari la Zimamoto na Uokoaji

Halmashauri ya Chalinze imepokea gari la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya kukabiliana na majanga punde yanapatokea wilayani hapo.

Gari hilo, limetolewa jana (23.08.2023) na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (SSF), Jenifa Shirima.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chalinze , Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, amemshukuru Mrakibu mwandamizi kwa niaba ya serikali kwa kuona kuwa katika mipango ya serikali Chalinze nayo iwe moja ya maeneo ya kipaumbele katika uhitaji wa gari hilo.

“Kufanikiwa kwa jambo hili nikufuatia muitikio wa kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Chalinze na majanga yaliyo wahi kuwakuta na ujio wa gari hili ni ukombozi mkubwa kwetu sote,” Mhe. Kikwete anasema.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi Mbunge wa jimbo hilo, Mrakibu Mwandamizi, Jenifa alimpongeza Mbunge huyo, Kikwete, kwa kuwasemea wananchi wake na kuongeza kwamba gari hilo ni utekeleza wa maombi ya Mbunge na Naibu Waziri Kikwete.

Mrakibu amemuahidi Mbunge huyo kuendelea kutatua kero za zimamoto katika halmashauri zote mkoa na kwamba na pia kumshukuru Mkurugenzi mtendaji wa Chalinze kwa kuwapatia Kiwanja ambacho watajenga Jengo la Zimamoto la wilaya na ofisi zao.

“Mhe. Kikwete, napenda kukuhakikishia kuwa serikali inajipanga kwa ajili ya ujio wa gari kubwa la wilaya hiyo,” anasema.

Wananchi wa Chalinze kwa jumla yao wameishukuru Serikali kwa kutatua kero hii ya muda mrefu. Wameahidi kulitunza.

error: Content is protected !!